Chakiba Club

BISMILLAHI RAHMANI RAHIM

SABALKHERI WANGWANA NA WATUNZI WA KISWAHILI

Azma kuu ya kuanzishwa kwa chama hiki ni kukuza matumizi ya Kiswahili hapa shuleni, pamoja na kuibua na kuendeleza vipaji miongoni mwa wanafunzi. Vipaji hivi vinajumuisha usomaji wa habari, kughani mashairi, uandishi wa kazi mbalimbali, na nyanja nyingine za lugha na fasihi.

Chama hiki huwapa wanachama motisha na fursa ya kuendeleza vipaji vyao kwa kuwapokea wanafunzi wenye shauku ya kujifunza, kujiendeleza na kubobea katika nyanja mbalimbali za Kiswahili.

Tangu kuanzishwa kwa chama hiki, mafanikio mengi yameafikiwa, ikiwemo matokeo bora katika somo la Kiswahili, hasa katika mtihani wa kitaifa. Mafanikio haya yanatupa matumaini na ari ya kufanya vizuri zaidi.

Tunatarajia kupata matokeo bora zaidi katika somo la Kiswahili mwaka huu, 2026. Kwa hivyo, ningependa kuwapa changamoto wanafunzi wote wajitahidi kutumia Kiswahili sanifu katika mawasiliano yao ya kila siku na kupunguza matumizi ya lugha ya Sheng shuleni.

Tuilinde, tuitumie na tuitangaze Kiswahili chetu!

Asanteni kwa kunisikiliza.