Shairi

Shairi

SIFA KWA MAMA

Furaha kuwajia, kuzaliwa kwangu pia,

Baraka kuwashukia, machozi kukaukia,

Zote zake Maulana,kumpataia nguvu mama,

Je ni nani kama mama, kwenye ulimwengu huu.

Chakula kunipatia, chenye lishe zote bora,

Asubuhi kuniamsha, na kuniandaa vyema,

Kwa usafi unaofaa, kama kinga ya magonjwa,

Je ni nani kama mama, kwnya ulimwengu huu.

Mateso yote kupita, na yote kupuuzia,

Na bado kunijalia, kwangu kuninyenyekea,

Kutosikia ya dunia, kumfanya kwake kusonga

Je ni nani kama mama, kwenye ulimwengu huu.

Mafanikio kujia, furaha kuwadia,

Maendeleo kupata, ya ndani ya familia,

Upendo kunionesha, na uvivu kuuzika,

Je ni nani kama mama, kwenye ulimwengu huu.

Namshukuru Maulana, kwa kunifikisha hapa,

Yote tisa ninasema, kumi nikimlizia,

Sita sita kunenea, sifa zake zote mama,

Je ni nani kama mama, kwenye ulimwengu huu.