Bismillahi, sabalkheri wangwana na watunzi wakitunzao Kiswahili. Azma kuu ya kubuniwa kwa chama hiki ni kukuza Kiswahili hapa shuleni na pia talanta miongoni mwa wanafunzi kama vile usomaji wa habari, kughani mashairi na uandishi wa nakala.
Hivyo, chama hiki huwapa motisha wanachama na kuinua talanta kwa kuwapokea walio na haja ya kujiendeleza na kubobea katika nyanja mbalimbali. Tangu kubuniwa kwa chama hiki, mafanikio mengi yameafikiwa kama vile matokea bora katika somo la Kiswahili hasa mtihani wa kitaifa.
Tunatarajia matokea bora zaidi katika somo la Kiswahili mwaka huu (2019). Ningependa kuwapa changamoto wanafunzi wote kutumia Kiswahili sanifu na kuangamiza lugha ya ‘Sheng.’
WALEZI WA CHAMA
Bi Rachael K
Bi Doreen K
Bi Naomi
Bw Mungai P